Klabu ya Aston Villa imetuma ofa ya paund million 10, huko DW Stadium kwa minajili ya kutaka kumuhamisha winga wa kifaransa Charles N'Zogbia aliekua shujaa wa kuikoa Wigan msimu uliopita ilipokua ikichunguliwa shimo la kushuka daraja.
Ofa hiyo imetumwa kufuatia winga huyo mwenye umri wa miaka 25 kuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaohitajika kwa udi na uvumba katika utawala wa meneja mpya huko Villa Park Alex McLeish ambae bado anapingwa vikali na mashabiki wa klabu hiyo.
Sababu kubwa ya kufanywa hivyo imetokana na mipango ya klabu ya Liverpool ya kumsajili winga Stewart Downing kukamilika baada ya kukubali kutoa kiasi cha fedha kilichotangazwa na uongozi wa Aston Villa kama ada ya uhamisho wake.
Pia kutumwa ofa hiyo huko DW Stadium kunachangiwa na uhamisho wa Ashley Young aliesajiliwa na Man Utd mwishoni mwa mwezi uliopiota ambapo hivi sasa amejumuika na wachezaji wengine huko nchini Marekani walipokwenda kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.
Hii si mara ya kwanza kwa Alex McLeish kutaka kumsajili Charles N'Zogbia, kwani alitaka kufanya hivyo mwanzoni mwa msimu uliopita akiwa na klabu iliyoshuka daraja Birmingham city lakini hatua hiyo ilishindikana dakika za mwisho.

No comments:
Post a Comment