KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 19, 2011

BARCELONA WAAPA KURUDISHA MWANA WAO NYUMBANI.


Siku moja baada ya kushauriwa kuacha kasumba ya kujifikiria mara mbili katika suala la kumrejesha nyumbani kiungo na nahodha wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas, meneja wa mabingwa wa soka nchini humo pamoja na barani Ulaya kwa ulaya FC Barcelona Josep Pep Guardila Isala ameapa kulimaliza sakata hilo kwa kutimiza malengo aliyojiwekea.

Josep Pep Guardila Isala ametoa ahadi hiyo kufuatai ushauri uliotolewa jana na kiongozi alipewa nafasi ya kudumu ndani ya FC Barcelona Johan Cruyff ambae alizungumzia dukuduku lake la kushangazwa hatua za kusita za usajili wa kioungo huyo mwenye umri wa miaka 24.

Josep Pep Guardila Isala amesema katika kipindi kilichosalia hadi August 31 ambapo itakua mwisho wa usajili wanaamini kila kitu kitakua sawa na Cesc Fabregas atafanikiwa kurejea nyumbani kama wengi wanavyotarajia.


Hata hivyo amedai kwamba kwa sasa mazungumzo ya uhamisho wa Fabregas yanaendelea na upande wa Barcelona unawakilishwa na mkurugenzi wa michezo Andoni Zubizarreta, huku ikiaminiwa hakuna kitakacho haribika.


Meneja huyo alieweka historia ya kuchukua vikombe 11 kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita toka akichukue kikosi cha FC Barcelona, amesema mazungumzo hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza baada ya nia yao kumsajili Fabregas kushindwa kutimia kwa miaka miwili iliyopita.

Wakati hayo yakielezwa na Josep Pep Guardiola Isala, mwenye umri wa miaka 40, uongozi wa klabu ya Arsenal ukiongozwa na mtendaji mkuu Ivan Gazidis umeshatangaza dhamira ya kumbakisha Fabregas ikiwa ni sehemu ya kukamilisha mipango ya kumaliza ukame ya mataji msimu ujao.

No comments:

Post a Comment