KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 20, 2011

KWELI UTAMADUNI WA KIAFRIKA NI WA KIPEKEE.


Mshambuliaji kutoka nchini Senegal El-Hadji Diouf anahofiwa huenda akaingia katika kadhia kubwa na uongozi wa klabu Blackburn Rovers baada ya kushindwa kuripoti kambini kwa muda muafaka.

El-Hadji Diouf alitakiwa kuwasili katika kambi ya klabu hiyo ya nchini Uingereza toka majuma mawili yaliyopita lakini alishindwa kufanya hivyo pasipo kutoa sababu zozote, hatua Ambayo iliwalazimu viongozi wa Rovers kumsaka kwa njia ya simu bila mafanikio.

Kufeli kwa mawasilino kati ya pande hizo mbili kulizusha mpango wa kumsaka wakala wake na ndipo mafaniko yalipo patikana huku jibu likitolewa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 atawasili kambini hii leo.

Kufikishwa kwa taarifa hizo huko Ewood park, kulimpa nafasi meneja wa Blackburn Rovers Steve Kean kuthibitisha taarifa hizo, ambazo bazo zilionekana kutowaridhisha walio wengi hatua mbayo itapelekea kuadhibiwa kwa El-Hadji Diouf.

Kikosi cha Blackburn Rovers, kilitarajia kuelekea nchini India kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa ligi, lakini safari hiyo imepigwa kumbo kutokana na sababu za kiusalama nchini humo.

Ikumbukwe kuwa Blackburn Rovers ni moja ya klabu zitakazoshiriki michuano ya Barclays Premier League Trophy itakayofanyika mjini Hong Kong nchini china kuanzia July 27 ambapo michuano hiyo bado itakua ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya.

Timu nyingine zitakazoshiriki michuano hiyo ni Kitchee ya nchini china, Chelsea pamoja na Aston Villa zote kutoka nchini uingereza.

No comments:

Post a Comment