KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, July 28, 2011

BLATTER AOMBA MUDA KUKOMESHA UCHAFU WA SOKA.


Raisi wa shirikisho la soka duniani kote FIFA Josep Sepp Blatter, ameomba kupewa muda katika harakati za kusafisha maovu yote yanayoendelea kufanywa na baadhi ya wadau wanaoutumia mchezo wa soka kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu.

Blatter ameomba nafasi hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari nchini Brazil alipokwenda kutazama maendeleo ya maandalizi ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambazo zitafanyika nchini humo.

Amesema FIFA wamejipanga kwa kila hali kumaliza uovu unaoendeshwa wa watu hao tena kwa kushirikiana na jeshi la polisi la kimataifa Interpol pamoja na taasisi mbali mbali ambazo zinajishughulisha na kuzuia uhalifu.

Amesema uovu unaoendelea katika mchezo wa soka unaofahamika na FIFA na kufanyiwa kazi, ni uchezaji wa kamari usio halali, ubaguzi wa rangi pamoja na upangaji wa matokeo.

No comments:

Post a Comment