KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, July 28, 2011

SAFARI YA BRAZIL UKANDA WA BARA LA AFRICA.


Shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA limetangaza utaratibu utakaotumika kwenye mpango wa kuzipata nchi tano za barani Afrika zitakazoshiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 zitakazofanyika nchini Brazil.

FIFA wametangaza utaratibu huo, huku ratiba kamili ya michezo ya kusaka nafasi ya kucheza fainali hizo ikitarajiwa kupangwa siku ya jumamosi mjini Rio de Janeiro nchini Brazil.

Katika mpango huo nchi ya Guinea Bissau, Equatorial Guinea, Chad, Swaziland, visiwa vya Comoro, Lesotho, Eritrea, Somalia, Djibouti, Mauritius, Visiwa Vya Sheli Sheli, pamoja na Sao Tome na Principe, ziwekwa katika kapu la sita na zitaingia katika hatua ya makundi ya barani Afrika baada ya kucheza michezo ya mtoano dhidi ya nchi zilizopo katika kapu la tano.

Nchi zilizowekwa katika kapu la tano ni Msumbiji, Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo, Togo, Liberia, Tanzania, Congo Brazzaville, Kenya, Rwanda, Ethiopia, Namibia, Burundi pamoja na Madagascar.

Hatua ya pili ya michezo ya awali ya fainali za kombe la dunia barani Afrika itazishirikisha nchi zilizoweka kwenye makapu manne tofauti ambapo katika kapu la kwanza linazijumuisha nchi zinazoshika nafasi kumi kwa ubora barani Afrika ambazo ni:
Ivory Coast, Egypt, Ghana, Burkina Faso, Nigeria, Senegal, Africa Kuisni, Cameroon, Algeria pamoja na Tunisia.

Kapu la pili linazijumuisha nchi zinazoshika nafasi ya 11-20 kwa ubora barani Afrika ambazo ni: Gabon, Libya, Morocco, Guinea, Botswana, Malawi, Zambia, Uganda, Mali pamoja na Visiwa vya Cape Verde.

Kapu la tatu linazijumuisha nchi zilizopo katika nafasi ya 21-28 kwa ubora barani Afrika ambazo ni: Benin, Zimbabwe, Jamuhuri ya Afrika ya kati, Sierra Leone, Sudan, Niger, Angola, pamoja na Gambia.

Kapu la nne linazijumuisha nchi kumi zitakazofanikiwa kupenya kwenye michezo ya hatua ya mtoano.

No comments:

Post a Comment