KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, July 28, 2011

Javier Hernandez Balcazer Chicharito NJE WIKI TATU.


Meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza Sir Alex Ferguson amesema huenda mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Mexico Javier Hernandez Balcazer Chicharito akawa nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua majuma matatu yajayo.

Sir Alex Ferguson amethibitisha taarifa hizo muda mchache mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya kikosi cha wachezaji wanaocheza ligi ya nchini Marekani uliochezwa mishale ya alfajiri kwa saa hapa nyumbani ambapo Man Utd waliibuka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri.

Amesema mshambuliaji huyo alipata mshutuko wa viungo wakati wa kupasha misulu kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa kirafiki uliochezwa nchini Marekani, hivyo jopo la madaktari litajitahidi kumfanyia matibabu.

Kukosekana kwa mshambuliaji huyo katika mchezo huo, kulimpa nafasi mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Bulgaria Dimitar Berbatov kujumuishwa kikosini na kufanikiwa kupachika moja ya mabao manne ya ushindi.

Mabao mengine yalipachikwa wavuni na Ji Sung Park, Danny Welbeck pamoja na Anderson.

Wakati huo huo kiungo Michael Carrick amesema maandalizi ya msimu mpya wa ligi wanayoendelea kuyafanya huko nchini Marekani yanawapa ari na nguvu huku akimini mengi yanafuata kutoka kwa meneja wao Sir Alex Ferguson kabla mchezo wa kuwania ngao ya hisani dhidi ya Man City utakaochezwa August 7 jijini London.

No comments:

Post a Comment