KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 5, 2011

Bojan Krkic KUICHEZEA AS ROMA.


Mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini humo pamoja na barani ulaya kwa ujumla FC Barcelona Bojan Krkic amekubali mpango wa kuihama klabu hiyo na kujiunga na AS Roma ya nchini Italia.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amekubali mpango wa kuelekea nchini Italia baada ya kuafikiana masuala la kimaslahi na viongozi wa klabu ya AS Roma ambao umefanikisha azma hiyo kupitia kwa meneja wao mpya Luis Enrique.

Hatua ya Bojan Krkic kukubalia kujiunga na FC Barcelona, inavunja mipango ya Spurs ya kutaka kumsajili, kwa kutumia kigezo cha kutemwa kwenye utarartibu wa meneja wa Barcelona Josep Pep Guardiola Isala ambae hatotaka kumtumia katika mikakati yake ya msimu ujao.

Kwa mantiki hiyo sasa Bojan Krkic ambae alikua mmoja wa wachezaji walioipa ubingwa wa Ulaya timu ya taifa ya vijana ya nchini Hispania chini ya umri wa miaka 21 kwa kuifunga timu ya taifa ya Uswiz katika mchezo wa fainali, anatarajia kuelekea mjini Roma wakati wowote kuanzia kesho tayari kwa kupimwa afya yake.

Bojan akiwa na klabu ya Barcelona toka mwaka 2007 tayari ameshacheza michezo 103 na kufunga mabao 26.

No comments:

Post a Comment