KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 5, 2011

Steven Gerrard KUACHWA KATIKA SAFARI YA BARANI ASIA.


Nahodha na kiungo wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard, hatojumuika na wachezaji wa klabu hiyo kwenye ziara ya barani Asia, ambayo itatumiwa na meneja King Kenny Dalglish kama sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Steven Gerrard, ataachwa kwenye safari hiyo ya siku ya jumapili baada ya kuonekana anahitaji muda wa kufanya mazoezi mepesi ambayo yatamrudisha katika hali yake ya kawaida kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi kati kati ya mwezi ujao.

Kiungo huyo kwa sasa ameshapona jeraha la nyonga ambalo lilimuweka nje kabla ya kumalizika kwa msimu wa mwaka 2010-11 ambao ulishuhudia Liverpool wakimaliza katika nafasi ya sita kwenye msiamo wa ligi.

Akithibitisha taarifa za kubaki kwa Steven Gerrard, meneja wa klabu ya Liverpool King Kenny Dalglish amesema anaamini kwa kipindi watakachokuwa barani Asia, kiungo huyo atapata muda wa kutosha wa kufanya mazoezi mepesi na watakaporejea tayari kwa michezo ya ligi huenda wakawa nae katika mchezo wa kwanza.

Kwa upande wake Steven Gerrard amesema kwa sasa anaendelea vyema, na mipango ya kuanza mazoezi mepesi anaichukulia kama sehemu mpya wa changamoto ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi baada ya kuwa nje ya uwanja toka mwezi March mwaka huu.

Hata hivyo amedai kwamba alikua na matarajio makubwa ya kujumuika na wachezaji wengine safarini, lakini ushauri uliotolewa na madaktari wa klabu ya Liverpool hana budi kuuheshimu na kuufuata kwa lengo la kujipa muda wa matayarisho.

No comments:

Post a Comment