KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 5, 2011

Carlos Tevez AIBUA UPYA SUALA LA KUHAMA CITY.


Mshambuali kutoka nchini Argentina Carlos Tevez ameendelea na mpango wake wa kutaka kuihama klabu ya Man city ambayo ilimsajili akitokea Man Utd misimu miwili iliyopita.

Carlos Tevez ambae kwa sasa yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kinachoshiriki fainali za mataifa ya bara la Amerika ya kusini, ameendeleza mpango huo huku akitoa sababu za kutaka kuwa karibu na familia yake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amesema tayari ameshawasiliana na mwenyekiti wa klabu ya Man city Khaldoon Al-Mubarak na kumuarifu taarifa hizo ambazo anaamini ipo siku zitakamilika na kutimiza malengo aliyojiwekea.

Amesema hatua ya kuwa mbioni kuondoka City Of Manchester isichukuliwe vibaya na mashabiki wa klabu hiyo pamoja na baadhi ya viongozi, bali inatakiwa kupokelewa kama sehemu ya kuheshimu maamuzi yake ambayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na hitaji la familia yake ambayo ina watoto wawili wa kike.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Boca Juniors ameendelea kusisitiza kwamba siku zote anapenda kuwafurahisha watoto wake ambao kwa kipindi kirefu ameishi nao mbali na endapo ataendelea kuishi nchini Uingereza anahisi atajiingiza katika kadhia kubwa ya msongo wa mawazo.

Hata hivyo inahisiwa kwamba Carlos Tevez yu njiani kuondoka Man City, kufuatia hali ya kutoelewana na meneja wa klabu hiyo Roberto Mancini ambae mara kwa mara wamekua wakikosana kauli na kupelekea hatua ya kushindwa hata kusalimiana.

No comments:

Post a Comment