KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 12, 2011

CARLOS TEVES KURUDI ALIPOTOKA.


Wakala wa mshambuliaji kutoka nchini Argentina Carlos Tevez amethibitisah taarifa za mchezaji huyo kuwa mbioni kusajiliwa na klabu yake ya zamani ya nchini Brazil Corinthians FC.

Kia Joorabchian wakala wa mshambuliaji huyo alieisaidia klabu ya Man City kumaliza ukame wa kukosa mataji kwa kipindi cha miaka 33 baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la FA msimu uliopita amesema tayari uongozi wa Corinthians FC umeshakubali kutoa ada ya uhamisho wa 35.

Kia Joorabchian amesema uongozi wa klabu hiyo ya nchini Brazil umekua ukifanya nae mawasiliano na umeonyesha kuwa tayari kutoa kiasi hicho cha pesa bila kipingamizi hatua ambayo anaamini itamaliza kiu ya Carlos Teves ya kuhama Man City na kuwa karibu na familia yake.

Amesema lengo lake yeye kama mtu wa karibu na mchezaji huyo ni kutaka kumuona Carlos Tevez anakua mwenye furaha wakati wote na hatojisikia vizuri endapo ataemuona anaendesha maisha yake kwa msukumo wa kutopenda mazingira yanayomzunguuka.

Hata hivyo pamoja na kuthibitisha taarifa hizo bado Kia Joorabchian akasema tayari kuna baadhi ya vilabu vya soka vya nchini Hispania pamoja na Italia vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Carlos Tevez lakini ofa zao hazilingani na ile iliyotangazwa na Corinthians FC.

Carlos Tevez kabla hajaanza kuishi barani ulaya mara baada ya kusajiliwa na West Ham Utd mwaka 2006, aliwahi kuitumikia Corinthians FC kuanzia mwaka 2004 ambapo akiwa na klabu hiyo aliwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa bara la Amerika ya kusini mara mbili mfululizo nah ii ilikuwa mwaka 2004 na 2005.

Kwa mara ya kwanza Carlos Tevez mwenye umri wa miaka 27 alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Amerika ya kusini mwaka 2003 akiwa mchezaji wa klabu ya Boca Junior ya nchini kwoa Argentina.

No comments:

Post a Comment