
Klabu ya Tottenham Hotspur imewazidi keta wapinzani wao kutoka jijini Londoin Chelsea, kufuatia kukamilisha usajili wa aliekua kinda wa klabu bingwa nchini Hispania pamoja na barani Ulaya kwa ujumla FC Barcelona Cristian Ceballos.
Spurs wamefanikisha azma hiyo ya kumsajili Cristian Ceballos mwenye umri wa miaka 18, baada ya kumfanyia majaribio kwa siku chache baada ya mchezaji huyo kufanyiwa hivyo na klabu ya Chelsea iliyokua kwenye mipango ya kukamilisha dili la kumsainisha mkataba.
Chelsea walimnasa mchezaji huyo, mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kutemwa na Fc Barcelona na walianza kumfanyia majaribio katika kipindi hiki cha maandalizi ya msimu lakini mipango ya zengwe iliyofanywa na Spurs ilifanikiwa kumteka na kufifisha matumaini ya kusajiliwa huko Stamford Bridge.

Katika hatua nyingine menaja wa kikosi cha Tottenham Hotspur Harry Redknapp amekua mzito kulizungumzia sakata la kiungo mshambuliaji Luca Modric anaehusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ya Chelsea.
Harry Redknapp ameonyesha uzito huo alipotakiwa kuzungumzia mustakabali wa Midric ndani ya kikosi chake ambacho msimu uliopita kilifanya vyema kwenye michuano ya kimataifa na kufika katika hatua ya robo fainali.
Amesema suala la mchezaji huyo ni zito na linapaswa kuzungumzwa na mwenyekiti wa klabu Daniel Levy ambae majuma mawili yaliyopita alifanya mkutano wa faragha na mchezaji huyo kutoka nchini Croatia lakini hata hivyo amekiri yu tayari kuendelea kumtumia katika kikosi chake.
No comments:
Post a Comment