KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 5, 2011

Paul Scholes AIPONDA ARSENAL.


Aliekua kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza pamoja na klabu ya Manchester United Paul Scholes ameziponda subra za washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal ambao kwa kipindi cha miaka sita sasa wameshindwa kutwaa ubingwa wa michuano yote walioshiriki.

Paul Scholes ameuponda mpango huo huku akisema, meneja wa klabu ya Man utd Alex Ferguson katu hawezi kuruhusu utaratibu huo wa kwenda kappa kwa kipindi cha miaka sita bila kikomb,e zaidi ya kubuni mbinu mbadala ya kusaka mafanikio.

Amesema anashangazwa na subra za mashabiki na uongozi wa klabu ya Arsenal ambayo imekua ikionyesha soka safi wakati wote na mwisho wa msimu kujikuta wakiambulia patupu na pengine kupelekea kuwapoteza wachezaji wazuri unapofika wakati wa usajili kama hivi sasa.

Wakati huo huo aliekua beki wa pembeni wa klabu ya Arsenal Gael Clichy, ambae jana alikamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Man City amesema haikuwa rahisi kufanya maamuzi ya kuihama klabu hiyo zaidi ya kuushinda unazi alionao moyoni.


Gael Clichy amesema aliipenda na kuithamini Arsenal ambayo imemtambulisha katika ulimwengu wa soka lakini ameona umewadia wakati wa kubadili mazingira na kupata changamoto mpya ya soka lake.

Amesema Arsenal ni klabu yenya timu nzuri lakini imekua ikishindwa kufikia malengo yake kutokana na baadhi ya mipango kutokukamilishwa, kama ya kuwasajili wachezaji ambao watatumika kama sehemu ya mbadala wa wachezaji wengine.

Wakati huo huo mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Kenny Sansom amekiri kuwepo kwa mapungufu makubwa katika kikosi cha Arsene Wenger ambacho kinakosa wachezaji wenye sifa ya kupigania mafanikio hadi mwisho wa msimu.

Amesema tatizo hilo halina budi kurekebishwa huko Emirates kama mafanikio yanahitajika, na kama utaratibu wa sasa utaendelezwa na meneja huyo kutoka nchini Ufaransa, bado ukame wa vikombe utashamiri kwa kipindi kingine kirefu.

No comments:

Post a Comment