KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 27, 2011

Charles N'Zogbia KUFANYIA VIPIMO VILLA PARK.


Mshambuliaji wa kifaransa Charles N'Zogbia hii leo alitarajiwa kupimwa afya yake tayari kwa kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Aston Villa akitokea Wigan Athetics.

Charles N'Zogbia alitarajiwa kuelekea mjini Birmingham kukamilisha utaratibu huo kufuatia mazungumzo ya viongozi wa Aston Villa dhidi ya wale wa Wigan kukamilika kwa makubaliano ya ada ya uhamisho wa paund million 9.5.

Hata hivyo imeelezwa kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atasaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia The Villians ambao utamuweka huko Villa Park hadi mwaka 2016.

Kabla ya taarifa za kuelekea mjini Birmingham hazijathibitishwa rasmi, Charles N'Zogbia, alikua mjini Dubai sanjari na kikosi cha Wigan kinachojiandaa na msimu mpya wa ligi chini ya meneja Roberto Martinez.

Kwa mantiki hiyo sasa Charles N'Zogbia, atakapokamilisha dili ya kujiunga na Aston Villa, atalazimika kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wengine klabuni hapo juma lijalo, kufuatai hivi sasa kikosi cha The Villians kuwa ziarani mjini Hong Kong kikishiriki michuano ya Barclays Asia Trophy iliyoanza hii leo.

Meneja wa Aston Villa Alex McLeish alitilia mkazo suala la kusajiliwa kwa N'Zogbia, baada ya kuondoka kwa mawinga wawili klabuni hapo ambao ni Ashley Young aliejiunga Manchester United pamoja na Stewart Downing aliejiunga na Liverpool katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa ligi.

No comments:

Post a Comment