KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 27, 2011

DAVID GILL AFUCHUA SIRI YA FERGUSON ILIYOKUA IMEFICHWA.

Mtendaji mkuu wa klabu bingwa nchini Uingereza Manchester United David Gill ametibua mipango ya meneja wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson, ya kuweka wazi suala la usajili mara baada ya kuwasajili wachezaji watatu katika kipindi hiki.

David Gill, amesema bado wanahitaji kufanya usajili wa mchezji mmoja ambae ataziba nafasi iliyoachwa wazi na kiungo alietangaza kustahafu soka mwishoni mwa mwezi May baada ya kuitumikiwa Man utd kwa kipindi cha miaka 12 mfululizo Paul Scholes.

Amesema bado hawajatambau ni wapi watakapotega mitego ya kumnasa mchezaji atakaeweza kuziba pengo la Scholes lakini amewatajka mashabiki wa mashetani wekundu kutambua kuwepo kwa mipango hiyo ya usajili.

Kauli ya David Gill imekuja zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya Sir Alex Ferguson kusema hana mpango ya kufanya usajili wa mchezaji mwingine, zaidi ya wachezaji watatu aliowasajili katika kipindi hiki ambao ni Ashley Young, Phil Jones pamoja na kipa David De Gea.

Wakati huo huo wakala wa mshambuliaji wa AS Roma Mirko Vucinic amesema kuna uwezekano wa mchezaji wake akasajiliwa na Manchester United.

Alessandro Lucci wakala wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amesema tayari ameshakutana na viongozi wa Man Utd lakini bado hawajafikia makubaliano ya uhamisho wa kumtoa huko nchini Italia.

Hata hivyo wakala huyo amdai kwamba, uongozi wa Juventus nao una mipango ya kutaka kumsajili Mirko Vucinic ambae tayari ameshaitumikia AS Roma kwa kucheza michezo 147 na kupachika mabao 46.

No comments:

Post a Comment