KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 27, 2011

Sergio Aguero ATUA MJINI MANCHESTER.


Hatimae dili la uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Sergio Aguero la kujiunga na mabingwa wa kombe la FA Man City linakaribia ukingoni baada ya kuwasili mjini Manchester hii leo.

Sergio Aguero ambae kwa sasa anashikiliwa na klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania, amewasili mjini humo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya ikiwa ni sehemu ya kukamilishwa kwa uhamisho wake ambao utaigharimu Man city kiasi cha paund million 40.

Kabla ya kufikia hatua ya kufanyiwa vipimo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, alitarajiwa kuketi chini na viongozi wa Man city kwa ajili ya kukubaliana masuala ya kimaslahi ambayo yataainisha ni kiasi gani atakua akilipwa kama mshahara wake kwa juma.

Safari ya mshambuliaji huyo kuelekea nchini Uingereza hii leo imekamilika ikiwa ni baada ya siku mbili ambazo zilishuhudia meneja wa Man City Roberto Mancini akathibitisha kuendelea kwa mazungumzo kati ya uongozi wa Atletico Madrid dhidi ya uongozi wa Man City.

Tayari meneja wa Atletico Madrid Gregorio Manzano amethibitisha utaratibu wa kukubali kumpoteza Sergio Aguero ambae alishindwa kuripoti kambini mwishoni mwa juma lililopita kama ilivyotarajiwa na wengi klabuni hapo baada ya kumaliza majukumu la kitaifa huko nchini Argentina.

Sergio Aguero anaelekea Man City kwa lengo la kuziba nafasi inayoachwa wazi na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez alieshupalia suala la kuondoka klabuni hapo, huku taarifa zikieleza kwamba huenda akajiunga na mabingwa wa dunia Inter Milan.

No comments:

Post a Comment