KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 27, 2011

URUGUAY WAPANDA VIWANGO VYA SOKA DUNIANI.

.
Mabingwa wapya wa fainali za mataifa ya bara la Amerika ya kusini COPA AMERIKA, Uruguay, wamepanda nafasi saba katika viwango vya ubora duniani na kushika nafasi ya tano.

Uruguay waliokua wakishika nafasi ya kumi na tatu, wamefanikisha azma ya kupanda katika viwango vya ubora duniani, kufuatia juhudi na mafanikio waliyoyapata kwenye fainali za COPA AMERIKA zilizofanyika nchini Argentina na kutwaa ubingwa kwa mara ya kumi na tano.

Uruguay ambao pia walifika katika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia mwaka 2010 kule nchini Afrika kusini, walinyakua ubingwa wa COPA AMERIKA mwishoni mwa juma lililopita kufuatia ushindi wa mabao matatu kwa sifuri uliopatikana mbele ya Paraguay.

Mabingwa mara tano wa fainali za kombe la dunia Brazil, ambao waliishia katika hatua ya robo fainali ya COPA AMERIKA mwaka huu, wao wamepanda kwa nafasi moja kutoka nafasi ya tano hadi ya nne.

Wenyeji wa fainali za COPA AMERIKA, Argentina wameendelea kusalia katika nafasi ya kumi, huku mabingwa wa Amerika ya kati na kaskazini Mexico wakianguka kwa nafasi kumi, kutoka nafasi ya kumi hadi katika nafasi ya 20, baada kushindwa kufanya vyema kwenye michuano ya COPA AMERIKA ambayo ilishuhudia wakiondoshwa bila kupata point hata moja.

Kusogea kwa nchi za Uruguay pamoja na Brazil, kunawafanya mabingwa wa dunia wa mwaka 1966 Uingereza kushuka kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya nne hadi ya katika nafasi ya sita.

Mabingwa wa dunia Hispania bado wanaendelea kupeta kileleni, wakifuatiwa na Uholanzi na nafasi ya tatu ikishindwa na Ujerumani.

Kumi bora za viwango vya soka duniani kwa mwezi huu wa saba:
1-Spain, 2-Netherlands, 3-Germany, 4-Brazil, 5-Uruguay, 6-England, 7-Ureno, 8-Italy, 9-Croatia, 10-Argentina.

No comments:

Post a Comment