KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 25, 2011

DILI LA Charles N'Zogbia LAREJESHWA MEZANI.


Hatimae uongozi wa klabu ya wigan umekubali kurejea mezani kuzungumza na uongozi wa klabu ya Aston Villa kwa ajili ya kukamilisha dili la usajili wa winga wa kimataifa toka nchini Ufaransa Charles N'Zogbia.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yalivunjika majuma matatu yaliyopita kufuatia uongozi wa Aston Villa kugoma kuongeza ofa ya usajili wa mchezaji huyo ambayo ililenga kumpeleka Villa Park kwa gharama ya paund million 9.

Taarifa zilizopatikana kutoka DW Stadium zimeeleza kwamba Aston Villa wamekubali kuongeza ofa yao na kufikia paund million 9.5 hatua ambayo imeufanya uongozi wa Wigan kurejea mezani kwa ajili ya kumaliza utaratibu wa uhamisho wa Charles N'Zogbia.

Juma lililopita meneja wa Aston Villa Alex McLeish aliapa mbele ya waandishi wa habari wakati akimtambulisha kipa Shy Given, kutokua tayari kuongeza dau la uhamisho wa Charles N'Zogbia, lakini kiapo chacke kimekwenda kinye na jinsi alivyokua amejipangia.

Charles N'Zogbia anahitajika kwa udi na uvumba huko Villa Park kufuatia kuondoka kwa mawinga wa klabu hiyo Ashley Young aliejiunga na Man Utd pamoja na Stewart Downing aliejiunag na Liverpool.

Kwa sasa Charles N'Zogbia amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja na tayari ameshagoma kusaini mkataba mpya wa kuitumikia klabu ya Wigan, hivyo viongozi wa The Latics wanahofia huenda akaondoka akiwa kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu ujao.

No comments:

Post a Comment