KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 25, 2011

DILI LA Javier Pastore LAVAMIWA NA PSG.


Mikakati ya klabu ya Chelsea ya kutaka kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini Argentina Javier Pastore imevamiwa na uongozi wa Paris St Germain *PSG* ya nchini Ufaransa.

Taarifa za mikakati hiyo ya Chelsea kuvamiwa, zimetangazwa rasmi na makamu wa raisi wa klabu ya Parlemo inayomuhodhi mchezaji huyo Guglielmo Micciche ambapo amesema wamepokea ofa kutoka PSG.

Amesema ofa hiyo waliyoipokea haina tofauti kubwa na ile iliyotumwa klabuni hapo na Chelsea, hivyo wataketi chini na kufikia muafaka na mchezaji ambae ndie muhusika kwa kusikia ni wapi angependa kucheza soka lake mara baada ya kuondoka nchini Italia.

Guglielmo Micciche amebainisha wazi kwamba raisi wa Parlemo Maurizio Zamparini, nae amebariki utaratibu huo ambao utakua ni wa demokrasia kwa kila anaehuska klabuni hapo kwenye harakati za uhamisho wa Pastore.

Uongozi wa Parlemo umesema huenda dili la uhamisho wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 likakamilishwa ndani ya juma hili.

Wakati huo huo meneja wa klabu ya chelsea Andre Villas Boas amesema hana pupa ya kufanya usajili kama mashabiki wengi wa klabu hiyo wanavyotaka kwa hivi sasa.

Villas Boas ametoa msimamo huo mara baada ya mchezo wa jana wa kirafiki dhidi ya kikosi maalum cha nchini Thailand ambacho kilikubali kisago cha mabao manne kwa sifuri yaliyofungwa na Frank Lampard, Jose Bosingwa, Branislav Ivanovic pamoja na Florent Malouda.

Amesema sera ya kufanya usajili kwa klabu hiyo ya London ipo pale pale na ataitimiza kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili mwishoni mwa mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment