KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, July 28, 2011

El-Hadji Diouf AFUNGWA JELA MIAKA MITANO.


Shirikisho la soka nchini humo limetangaza kumfungia mshambuliaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo pamoja na klabu ya Blackburn Rovers ya nchini Uingereza El-Hadji Diouf kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia hii leo.

Shirikisho la soka nchini Senegal limefikai maamuzi hayo kufuatia kauli iliyotolewa na El-Hadji Diouf, katika moja ya redio za nchini Ufaransa ambapo alidai kwamba mfumo wa uendeshaji soka barani Afrika umetawaliwa na rushwa.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo El-Hadji Diouf, alitakiwa na kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka nchini Senegal kuwasilisha uthibitisho wa kauli alitoitoa mbele ya kamati July 20, lakini alishindwa kufanya hivyo hatua ambayo imechukuliwa kama ukaidi.

Ufafanuzi uliotolewa juu ya adhabu ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 unaonyesha kwamba kwa kipindi cha miaka mitano, hatoruhusiwa kujishughulisha na shughuli zozote za mchezo wa soka ndani ya nchi ya Senegal.

Mbali na adhabu hiyo El-Hadji Diouf, pia anakabiliwa na adhabu kali ya kukatwa mshahara wake kwa juma katika klabu yake ya Blackburn Rovers, kufuatia kushindwa kuripoti kambini kwa muda aliopangiwa na badala yake alifanya hivyo kati kati ya juma lililopita.

Meneja wa klabu hiyo Steve Kean tayari ameshathibitisha taarifa za kuadhibiwa kwa mshambuliaji huyo kufuatia sakata linalomkabili.

No comments:

Post a Comment