KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, July 28, 2011

NIGERIA KUCHEZA TENA NA RAGENTINA.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Samson Siasia amekubali kikosi chake kucheza mchezo mwingine wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Argentina ambayo ilikua mwenyeji wa fainali za mataifa ya Amerika ya kusini zilizomalizika mwishoni mwa juma lililopita huko mjini Buenos Aires.

Samson Siasia amekubalia kuchezwa kwa mchezo huo kwa lengo la kutaka kuutumia kama sehemu ya kukipa maandalizi kikosi chake ambacho kinaendelea na harakati za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 2012.

Amesema mchezo huo utachezwa September 6 mwaka huu, mjini Dhaka nchini Bangladesh na hii itakua mara tu baada ya mchezo wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika dhidi ya Madagaster ambao utaunguruma mjini Antananarivo September 4.


Kocha huyo ambae pia aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, amesema bado anaamini kikosi chake kitathibisha uwezo wa kuifunga tena timu ya taifa ya Argentina, ambayo mwezi uliopita ilikubalia kisago cha mabao manne kwa moja.

Timu ya taifa ya Nigeria bado ina hali ngumu ya kujihakikishai nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 2012 kufuatia ugumu wa wa kundi la pili linalozijumuisha nchi kama Guinea, Ethiopia pamoja na Madagascar.

No comments:

Post a Comment