KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 29, 2011

UEFA WASIKILIZA RUFAA YA MOURINHO.


Kamati ya rufaa ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, hii leo imesikiliza rufaa iliyowasilishwa na meneja wa Real Madrid Jose Mourinho ya kupinga adhabu ya kufungiwa michezo mitano iliyo chini ya shirikisho hilo.

Rufaa hiyo imesikilizwa huku Jose Mourinho akipata nguvu ya kutosha kutoka kwa viongozi wa Real Madrid ambao wamekua bega kwa bega na meneja huyo toka nchini Ureno ambae anaaminiwa huenda akaleta mabadiliko huko Estadio St Bernabeu.

Kabla ya hapo kamati ya maadili ya shirikisho hilo ilitangaza kumuadhibu Jose Mourinho, kwa kutokukaa katika benchi la ufundi la klabu yake sanjari na kumtoza fainali ya paund 71,917 ambazo ni sawa na Euro 50,000.

Hata hivyo bado haijafahamika nini ambacho kimeamuliwa katika kikao cha kamati ya rufaa ya UEFA ambayo kutwa nzima hii leo imekua katika kikao kirefu.

Kama itakumbukwa vyema Jose Mourinho alikumbwa na adhabu hiyo baada ya kuamuriwa kukaa jukwaani na muamuzi aliechezesha mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu uliopita, ambao ulishuhudia mabingwa wa barani humo FC Barcelona wakiiadhibu Real Madrid kwa kuifunga mabao mawili kwa sifuri.

Sababu kubwa ya Mourinho kutakiwa kuondoka katika benchi la ufundi ilitokana na kauli aliyomtolea muamuzi alichezesha mpambano huo kwa kumuekleza wazi anawabeba Barcelona, baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa beki wake kutoka nchini Ureno Pepe, ambae alidaiwa kumfanyia rafu mbaya mshambuliaji David Villa.

Licha ya kuadhibiwa huko, bado Jose Mourinho alizungumza maneno makali katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alidai Barcelona kila mara wamekua wakibebwa na waamuzi na huenda wamekua wakifanyiwa hivyo kutokana na kuwa chini ya waliokua wadhamini wao shirika la kuhudumia watoto duniani Unicef.

No comments:

Post a Comment