
Mabingwa wa kombe la FA Manchester City amedhamiria kukamilisha usajili wa beki wa pembeni wa klabu ya Arsenal Gael Clichy ambaetayari ameshaonyesha lengo la kutaka kuihama klabu hiyo ya jijini London katika kipindi hiki baada ya kugoma kusaini mkataba mpya.
Man City wamedhamiria kukamilisha usajili wa mchezaji huyo wa kifaransa, hukua kijinadi kuwa tayari kutoa kiasi cha paund million 7 kama ada ya uhamisho wake hatua mabyo inaifuta ndotoz a klabu ya Liverpool ambayo iluikua imejipanga kutoa kiasi cha paund million 5.
Matumaini mengine ambayo yanaonyesha ni vipi Man City huenda wakampata beki huyo ni dau la mshahara walilolitangaza, ambapo Gael Clichy endapo atakubali kujiunga na klabu hiyo ya mjini Manchester atakua akilipwa paund elfu 90 kwa juma tofauti an anavyolipwa hivi sasa na klabu yake ya Arsenal ambayo kila juma imekua ikimlipa mshahara wa paund elfu 50.
Hatya hivyo bado meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameendelea kushikilia msimamo wake wa kumbembeleza mchezaji huyo ili akubali kusaini mkataba mpya ili aweze kusalia kikosni kufuatia kuhitajika kwa hali na mali katika mipango yam zee huyo wa kifaransa.
Wakati huo huo imefahamika kwamba, uongozi wa klabu ya Southampton umekubali kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Arsenal kwa ajili ya usajiliwa Alex Oxlade-Chamberlain.
Taarifa kutoka katika mkutano wa mazungumzo hao zinaeleza kwamba suala la ada ya uhamisho limekua kikwazo kikubwa na kupelekea hatua ya majadiliano ya muda mrefu.
Uongozi wa Southampton umeripotiwa kuwa tayarui kumuuza Alex Oxlade-Chamberlain kwa kiasi cha paund million 12, lakini Arsenal wanaomba kupungiziwa kiasi hicho cha fedha.
No comments:
Post a Comment