
Wakala wa mshambuliaji wa klabu ya Santos Neymar da Silva Santos Júnior amesema hazipi uzito taarifa za mchezaji huyo kuwa mbini kusajiliwa na klabu za barani Ulaya ambazo tayari zimekubali kutoa kiasi cha Euro million 45 ambacho kitatumika kama ada ya uhamisho wake.
Wagner Ribeiro, wakala wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19 amesema bado kuna uwezekano mkubwa kwa Neymar da Silva Santos Júnior kuendelea kubaki katika utawala wa klabu ya Santos kufuatia mipango ya viongozi wa klabu hiyo kuendelea kumuhitaji.
Wagner Ribeiro amesema hakuna anaepinga kusajiliwa na mchezaji huyoa mbae pia huitumikia timu ya taifa ya Brazil, ila kinachoonekana kwa sasa ni utaratibu wa mikakati ambayo inahisiwa ikifanywa sasa hivi itakuwa imemuharakisha Neymar da Silva Santos Júnior kuelekea barani Ulaya.
Siku mbili zilizopita raisi wa klabu ya Santos Luis Álvaro de Oliveira Ribeiro, alithibvitisha taarifa za klabu tano za barani ulaya ambazo zimekiri kuwa tayari kumsajili Neymar kwa kiasi cha Euro Million 45 kwa masharti ya kutozitaja klabu hiyo.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na vyoimbo vya habari ulimwenguni kote umebaini kwamba klabu hizo tano ni Real Madrid na Barcelona za nchini Hispania, Chelsea pamoja na Manchester City za nchini Uingereza na klabu Anzhi Makhachkala ya nchini urusi.
No comments:
Post a Comment