
Raisi wa klabu ya Palermo Maurizio Zamparini amethibitiusha taarifa za kutumwa kwa ofa ya klabu ya chelsea ya nchini Uingereza ambayo imemlenga kiungo mchezeshaji kutoka nchini Argentina Javier Pastore.
Maurizio Zamparini amesema wamepokea ofa hiyo ya paund million 45, lakini bado wanatazama kama unauwezekano wa kutumwa kwa ofa nyingine kutoka kwenye klabu nyingine ambazo tayari zilionyesha matamanio ya kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.
Amesema klabu kama Real Madrid imekua katika mfumo wa kutaka kumsajili Javier Pastore, ambae msimu uliopita alikua chachu ya kupatikana kwa mafanikio kwa klabu ya Parlemo ambayo itashiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Hata hivyo Maurizio Zamparini ameongeza kuwa klabu ya chelsea bado inapewa nafasi ya upendeleo kumsajili mchezaji huyo, ambae huenda akawa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na meneja mpya kutoka nchini Ureno Andre Villa Boas.
Javier Pastore, kwa sasa yupo nchini kwao Argentina akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kesho kitafungua michuano ya mataifa ya bara la Amerika ya kusini *Copa America* dhidi ya timu ya taifa ya Bolivia.
No comments:
Post a Comment