KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 29, 2011

Giuseppe Rossi KUBAKI VILLAREAL.


Wakala wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Italia Giuseppe Rossi, amesema kuna uwezekano mkubwa kwa mchezaji huyo kuendelea kuwepo huko El-Madriga Stadium licha ya kuhusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na kibibi kizee cha Turine Juventus.

Federico Pastorello wakala wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Man Utd, ameeleza kwamba, hatua za kibibi kizee cha Turine za kutuma ofa ya usajili huko El-Madriga, zimekua hazina muelekeo wa kuthibitisha kama kweli wanataka kumsajili Giuseppe Rossi.

Amesema mipango hiyo ya kutokueleweka, inaendelea kuwafanya viongozi wa Villareal kubadili mawazo ya kumuuza mshambuliaji huyo, ambae alikua katika fungu la wachezaji wanaouzwa katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa ligi.

Hata hivyo Federico Pastorello amedai kwamba kuuzwa kwa Santi Cazorla, aliejiunga na CF Malaga, napo kumechangioa kuanza kufikiria mipango ya kumtoa Giuseppe Rossi kwenye fungukla kuondoka huko El-Madriga.

Fedha za usajili wa Santi Cazorla ambazo ni Euro million 19 sawa na paund million 16.6, zinasemekana huenda zinawatosha viongozi wa Villareal kurekebisha kikosi chao kwa kufanya usajili wa wachezaji wengine, hatua ambayo imekwenda kinyume na hapo awali ambapo walidhani huenda wangehitaji pesa nyingi zaidi kukamilisha utaratibu huo ambao pia ulihitaji kuuzwa kwa Giuseppe Rossi.

No comments:

Post a Comment