KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 1, 2011

DOGO KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA UHOLANZI.


Kiungo kinda wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere, huenda akakosa nafasi ya kuitwa katika timu ya taifa ya Uingereza kufuatia maumivu wa kifundo cha mguu aliyoyapata jana akiwa katika mchezo wa pili wa michuano ya Kombe la Emirates huko jijini London.

Jack Wilshere ameibu fikra hizo, kufautia maelezo yaliyotolewa na meneja wa Arsenal Arsene Wenger katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya New York Red Bulls kutoka nchini Marekani na Arsenal kuambulia matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Arsene Wenger amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 huenda akawa nje ya uwanja hadi juma lijalo, hatua ambayo itamfanya kuukosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Uingereza dhidi ya washindi wa pili wa fainali za kombe la Dunia 2010 timu ya taifa ya Uholanzi.

Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Ufaransa amedai kwamba, bado kuna uwezekano mkubwa kwa Jack Wilshere kuwahi kurejea uwanjani, kufautia maelezo aliyohakikishia na jopo la madaktari klabuni hapo hivyo itatazamwa kama hatua hiyo itafanikiwa.

Wakati Jack Wilshere, akiwa katika hali ya sintofahamu, tayari kiungo na nahodha wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard pamoja na winga wa Arsenal Theo Walcott wameshaenguliwa kikosini kufautia mnajeraha yanayowakabili kwa sasa.

Wakati huo huo, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amepania kuipa mafanikio makubwa nchi hiyo kabla hajamaliza muda wake baada ya fainali za mataifa ya barani Ulaya zitakazofanyika mwakani huko nchini Ukraine pamoja na Poland.


Fabio Capello ameeleza mpango huo, wakati akifanyia mahojiano na kiutuo cha televisheni cha nchini kwao Italia ambapo amesema anaimani ataweza kufikia malengo hayo kutokana na umahiri wa kikosi chake kwa sasa.

Amesema hakuna linaloshindikana hasa ukizingatiwa kwamba nchi ya Uingereza imesubiri kwa kipindi kirefu kutwaa mataji, ambapo kwa mara ya mwisho kufanya hivyo ilikua mwaka 1966 katika fainali za kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment