KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 29, 2011

MALAYSIA WAIOMBA RADHI CHELSEA.

Chama cha soka nchini Malaysia kimeutaka radhi uongozi wa Chelsea kufuatia malalamiko yaliyotolewa jana na klabu hiyo ya jijini London ya kubaguliwa kwa kiungo Yossi Benayoun katika mchezo wa kirafiki dhidi ya kikosi maalum cha nchi hiyo uliochezwa juma lililopita.

Taarifa iliyowasilishwa huko Stamford Bridge kama sehemu ya kuomba radhi, imeeleza kwamba, pamoja na mamalalamiko waliyoyasikia bado hawana uhakika kama kweli kiungo huyo alibaguliwa kwa kuzomewa na mashabiki.

Taarifa hiyo imeendelea kubainisha kuwa, nchi ya Malaysia kuwa na asilimia kubwa ya waislamu haimaanishi kama kweli suala la ubaguzi kwa waisrael linapewa nafasi, zaidi ya kila mmoja kuamini imani yake.

Nchi ya Malaysia inaripotiwa kuwa na waislamu wanaofikia million 28, na imekua ikisemekana inawakubali sana wapalestina zaidi ya waisrael.

No comments:

Post a Comment