KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, July 28, 2011

CHELSEA WACHUKIZWA NA MASHABIKI WA MALAYSIA.


Uongozi wa klabu ya Chelsea umelaani kitendo cha mashabiki wa soka nchini Malaysia cha kumzomea kiungo wa kimataifa toka nchini Israel pamoja na klabu hiyo Yossi Benayoun wakati wa mchezo wa kirafiki uliounguruma juma lililopita mjini Kuala Lumper.

Chelsea umelaani kitendo hicho huku ukikiri kuchukizwa na tabia za mashabiki hao ambao walimzomea Yossi Benayoun kila alipopata nafasi ya kuumiliki mpira na hatua hiyo inahisiwa hunsda inatokana na utaifa wake.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo ya jijini London imeeleza kwamba, vitendo hivyo vya mashabiki, havistahili kufumbiwa macho katika mchezo wa soka na kama vitaachwa na kuendelea lengo la mchezo huo la kudumisha mahusiano halitatimia kamwe.

Nchi ya Malaysia imekua ikiwaunga mkono wapalestina kila kukicha na huenda sababu hiyo ikawa chanzo cha Yossi Benayoun, kupata mapokezi tofauti kutoka kwa mshabiki wa nchini humo ambao wanawapiga vita waisrael.

Licha ya kupokelewa vibaya huko nchini Malaysia, Yossi Benayoun aliendelea kupewa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Chelsea ambacho jana kiliibuka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri dhidi ya Kitchee FC ya nchini China kwenye michuano ya Barclays Asia Trophy.

Katika hatua nyingine meneja wa klabu ya Chelsea Andre Villas Boas amekiri kufurahishwa na mwenendo wa kikosi chake ambacho mpaka sasa kimefanikiwa kushinda michezo yote ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Amesema kazi ya maandalizi iliyofanyika ni kubwa na kwa kipindi kifupi hasa ukizingatia muda wa kuanza kwa michezo wa ligi unakaribia pamoja na ile ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment