KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 5, 2011

Luca Modric KUKUTANA BOSI MKUBWA WA KLABU.


Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Hotspurs Daniel levy hii leo alitarajia kukutana na kiungo mchezeshaji wa klabu hiyo Luca Modric anaehusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu za Chelsea pamoja na Man Utd.

Daniel Levy alitarajia kukutana na kiungo huyo kwa ajili ya kuweka mambo sawa ambayo yanahisiwa huenda yakawa kikwako kikubwa kwa Modric na kumsababishia kufikiria kuondoka katika kipindi hiki.

Katika mkutano huo kubwa ambalo lilitarajiwa kuzungumzwa ni suala la mkataba mpya pamoja na kuboreshwa kwa maslahi ya mchezaji huyo aliejiunga na Spurs mwaka 2008 akitokea nchini kwao Croatia lipokua akiitumikia klabu ya Dinamo Zagreb.

Wakati mazungumzo hayo yakipangwa kufanyika hii leo, tayari meneja wa Spurs Harry Redknapp ameshatoa msimamo wa kutokua tayari kumuuza Luca Modric pamoja na wachezaji wengine klabuni hapo.

Harry Redknapp ametoa msimamo huo akiwa kwenye mzoezi ya kikosi chake tayari kwa msimu mpya wa ligi ambapo amesema mpaka jana alikuwa na wachezaji 21 kikosini huku wachezaji wengine wakiwa katika majukumu ya timu za mataifa yao.

No comments:

Post a Comment