KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, July 20, 2011

LUCA MODRIC NA PIRIKA ZA KUHAMIA CHELSEA.


Kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspurs Luca Modric bado anazunguukwa na mazingira magumu ya kuihama klabu hiyo na kujiunga na majirani zao huko jijini London Chelsea wanaohitaji kumsajili kwa udi na uvumba.

Luca Modric bado yu katika mazingira hayo kufuatia kauli iliyotolewa na meneja wa Spurs Harry Redknap mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi dhidi ya mabingwa wa soka nchini Afrika kusini Orlando Pirates.

Harry Redknap amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 bado ana msaada mkubwa ndani ya kikosi chake na katu hatoi nafasi kwa yoyote kumsajili katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye ushindani wa michuano kadha wa kadha ya msimu ujao.

Amesema mengi yamezungumzwa na kuandikwa katika vyombo vya habari lakini anajua nini anachokifanya kufuatia mipango yake aliyojiwekea huko White Hart Lane.

Katika hatua nyingine Harry Redknapp akatetea maamuzi ya kumpa unahodha mchezaji huyo katika mchezo wa jana dhidi ya Orlando Pirates ambapo kulichukuliwa kama anambembeleza, kwa kusema si mara ya kwanza kufanya hivyo na kwa kawaida Modrid hupewa nafasi hiyo endapo nahodha Ledley King pamoja na msaidizi Michael Dawson hawatoanzishwa kikosini.

No comments:

Post a Comment