KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 29, 2011

MAN CITY YAPIGWA KIJEMBE !!


Meneja wa klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas ameudhiki utaratibu wa usajili unaoendelea kufanywa na Man City kwa kusema hauendani na hadhi ya klabu hiyo ya mjini Manchester.

Andre Villas-Boas amesema uongozi wa klabu hiyo ni kweli unajipanga kufanya makubwa katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza na pengine barani ulaya kwa ujumla lakini si kwa fedha nyingi wanazozitumia kwa ajili ya usajili.

Amesema klabu hiyo toka ilipokua chini ya taykun kutoka falme za kiarabu Sheikh Mansour bin Zayed bin Sultan Al Nahyan, imeshatumia kiasi kikubwa cha fedha lakini mpaka sasa imeambulia kombe la FA ambalo linaweza kuchukuliwa na klabu yoyote, kutokana na mtiririko wa ushindani wake.

Akitolea mfano wa klabu ya Chelsea meneja huyo aliechukua mikoba ya Carlo Ancelotti alietimuliwa mwezi May mwaka huu, amesema ni kweli klabui hiyo wa jijini London imetumia kiasi kikubwa cha pesa kwa kuwasajili wachezaji lakini tayari mafanikio yameonekana, ya kutwaa ubingwa wa nchini Uingereza ambao ulisubiriwa kwa muda wa miaka 50.

No comments:

Post a Comment