KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 25, 2011

MAN CITY WAKARIBIA KUMNASA Sergio Aguero.


Dalili za kuondoka kwa mshambuliaji kutoka nchini Argentina Sergio Aguero huko Stadio Vicente Calderon zinaendelea kushamiri kufautia kushindwa kuripoti kambini kama alivyotarajiwa.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, kwa kipindi hiki cha usajili amekua kwenye mlolongo wa kuhusika na taarifa za kuachana na klabu hiyo ya mjini Madrid na kuwa mboini kuelekea upande wa real Madrd ama kuvuka mipaka na kutinga katika klabu ya Man City.

Sergio Aguero alitakiwa kuripoti kwenye kambi ya kikosi cha Atletico Madrid jana jioni lakini suala hilo limeshindikana huku akishindwa kutoa sababu maalum kwa viongozi wa klabu hiyo.

Sergio Aguero alipewa muda mrefu wa kupumzika kufuatia ushiriki wa timu ya taifa lake katika michuano ya mataifa ya bara la Amerika ya kusini *COPA AMERICA* lakini bado ameonyesha kukaidi heshima aliyopewa.

Hata hivyo tayari Man city wanaonyesha kuwa mstari wa mbele kuhitaji saini ya mshambuliaji huyo ambapo meneja Roberto Mancini amekiri kuendelea kwa baadhi ya mipango ya uhamisho wa Sergio Aguero ambayo huenda ikamilika ndani ya siku saba zijazo.

Sergio Aguero anapewa nafasi ya kuelekea city of Manchester kufuatia nafasi itakayoachwa wazi na Carlos tevez ambae ameshaeleza nia yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment