KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 29, 2011

Marco Branca AMKANA CARLOS TEVEZ.


Mkurugenzi mkuu wa mabingwa wa soka duniani Inter Milan Marco Branca amemkana mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez ambae anadaiwa huenda akajiunga na klabu hiyo ya mjini Milan.

Marco Branca amemkana mshambuliaji huyo kufuatia taarifa zilizochapishwa katika magazeti ya nchini Uingereza juma lililopita ambapo taarifa zake zilidai kwamba kukutana kwao kisiwani Sardinia kulikua na siri kubwa ya mazungumzo ya kumtaka ajiunge na Inter Milan mara baada ya safari ya kuelekea nchini Brazil kuota mbawa.

Marco Branca amesema Carlos Tevez ni rafiki yake wa siku nyingi na kukutana kwao kisiwani Sardinia kusichukuliwa kama taarifa zilizoandikwa katika vyombo vya nchini Uingereza ambavyo amedai vinataka kumgombanisha na viongizi wa klabu ya Man City kupitia mshambuliaji huyo.

Amesema ni kweli walifanya mazungumzo na Carlos Tevez wakiwa kisiwani Sardinia lakini si mazungumzo ya kumshawishi kujiunga na Inter Milan bali yalilenga sana maisha yao binafsi.

Carlos Tevez, kwa sasa amekua na msimamo wa kutaka kuihama Man City kufautai kisingizio cha kuhitaji kuwa karibu na familia yake inayoishi nchini Argentina, hatua ambayo ilipelekea kuhusishwa na mipango ya kusajiliwa na Sports Club Corinthians Paulista ambayo hata hivyo ilifeli kutokana na muda wa usajili nchini Brazil kumalika bila mafanikio.

Hata hivyo kuondoka kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 huko Etihad Stadium, kwa sasa itakua ni lazima kutokana na kukamilishwa kwa usajili wa mshambuliaji Sergio Aguero akitokea Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho wa paund million 35.

No comments:

Post a Comment