
Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Valencia Braulio Vazquez amekanusha taarifa za kiungo kutoka nchini Argentina pamoja na klabu hiyo Ever Banega kuwa kwenye mipango ya kusajiliwa na klabu bingwa duniani Inter Milan ya nchini Italia.
Braulio Vazquez amesema mpaka sasa hakuna ofa yoyote walioipokea kutoka nchini Italia kama inavyoripotiwa na waamini Ever Banega atakapomaliza majukumu ya kitaifa nchini Argemntina atajiunga na wachezaji wengine kikosini tayari kwa maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
Amesema taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ya Inter Milan wao kama viongozi wamekua wakizisikia na kuziona kupitia vyombo vya habari na hatua hiyo haijawashtua kutokana na kufahamu kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 ni mali yao halali.
No comments:
Post a Comment