KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, July 28, 2011

Sergio Aguero ATANGAZA KUWA HALALI ETIHAD STADIUM.


Siku moja baada ya kuwasili mjini Manchester, mshambuliaji wa kimataifa toka nmchini Argentina Sergio Aguero amejitangaza hadharani kuwa mchezaji halali wa klabu ya Man city iliyo mbioni kukamilisha uhamisho wake akitokea Atletico Madrid ya nchini Hispania.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miuaka 23, ametangaza suala hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twiter ambapo amesema kwa sasa ana kila sababu ya kutambuliwa kama mchezaji halali wa klabu hiyo ya Etihad Stadium, kufuatua masuala yake binafsi na viongozi wa Man City kwenda vyema.

Amesema anajihisi mwenye furaha kuwa klabuni hapo toka jana, na pia amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata kutoka kwa mashabiki huku akimini yatampa nafasi nzuri ya kucheza kwa kujiamini na kutimiza malengo aliyojiwekea akiwa na klabu mpya msimu ujao.

Sergio Aguero ataihama Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho wa paund million 40, na siri kubwa ya kutaka kusajiliwa na Man City ni kuziba nafasi itakayoachwa wazi na mshambuliaji wenzake kutoka nchini Argentina Carlos Tevez.

Wakati huo huo mtendaji mkuu wa Sports Club Corinthians Paulista amesema bado hawajakatishwa tamaa na taratibu za kutaka kumsajili mshambuliaji Carlos Tevez baada ya kushindwa kufanya hivyo juma lililopita.

Amesema lengo lao kubwa la kutaka kumsajili Carlos Tevez lilikua ni kusaidiana na wachezaji wengine katika kipindi hiki cha ligi ya nchini Brazil, lakini pamoja na kumkosa bado wanaamini watafanya vyema kufuatia msimamo wa ligi unavyoonyesha.

No comments:

Post a Comment