KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 8, 2011

AFRICA YAPELEKA TIMU TATU KATIKA MZUNGUUKO WA PILI.


Timu ya taifa ya vijana ya Nigeria chini ya umri wa miaka 20, imefanikiwa kumaliza michezo ya hatua ya makundi ya fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Colombia kwa kuongoza kundi la nne.

Vijana hao wa Nigeria wamefikia mafananikio hayo baada ya kuichapa timu ya taifa ya Saudi Arabia mabao mawili kwa sifuri katika mchezo uliounguruma usiku wa kuamkia hii leo.

Mabao hayo ya ushindi yalipachikwa wavuni na Ahmed Musa pamoja na Olarenwaju Kayode na kuifanya Nigeria kufikia point tisa.

Kwa matokeo hayo sasa timu ya taifa ya Nigeria inasonga mbele na itacheza na timu ya taifa ya Uingereza katika mchezo wa mzunguuko wa pili utakaounguruma August 11.

Timu nyingine ya bara la Afrika iliyofanikiwa kusonga mbele katika fainali hizo za kombe la dunia ni Cameroon iliomaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi la pili na sasa itakutana na timu ya taifa ya Mexico mnamo August 11.

Nayo timu ta taifa ya vijana ya Misri imefanikiwa kutinga katika hatua ya pili ya fainali hizo ikipitia katika kundi la tano ambalo lilishuhudia timu hiyo ikimaliza katika nafasi ya pili.

Misri itapambana na Argentina mnamo August 10.

No comments:

Post a Comment