KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 24, 2011

Alberto Aquilani KURUDI NYUMBANI ITALIA.


Wakala wa kiungo kutoka nchini Italia na klabu ya Liverpool Alberto Aquilani, amesema kuna matumaini makubwa ya kukamilishwa kwa usajili wa mchezaji wake ambae anawaniwa mabingwa wa Sirie A AC Milan.

Franco Zavaglia, wakala wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, amesema mipango yote ya uhamisho inakwenda vyema na wakati wowote kabla ya August 31 itakua imekamilishwa na pande hizo mbili.

Hata hivyo amedai kwamba kwa sasa bado yupo mjini Liverpool, akishughulikia upande wa viongozi wa klabu hiyo ya Anfield na baada ya hapo ataelekea nchini Italia kukamilisha utarartibu mwingine ambao unatakiwa kumalizwa na AC Milan.

Amesema amekaa chini na Alberto Aquilani, ambapo amemueleza wazi nia yake ya kuwa tayari kurejea nyumbani kwao italia, kuitumikia AC Milan, baada ya kufanya hivyo msimu uliopita kwa kukubalia kuitumikia Juventus kwa mkopo.

Mpaka sasa ada ya uhamisho wa kiungo huyo ambae bado ana mkataba na klabu ya Liverpool hadi mwaka 2014 haijatangazwa, lakini inaaminiwa huenda ikafanywa kuwa siri endapo viongozi wa Liverpool na wale wa AC Milan watakubaliana suala hilo.

No comments:

Post a Comment