KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 24, 2011

Romelu Lukaku AKIRI ALIITAMANI CHELSEA KITAMBO.


Mshambuliaji mpya wa klabu ya chelsea Romelu Lukaku amekiri kufurahishwa na hatua ya kusajiliwa na klabu hiyo ya jijini London ambayo amekiri alikua ndoto za kuitumikia katika maisha yake.

Romelu Lukaku aliesajiliwa na The Blues akitokea katika klabu ya Anderlatch ya nchini Ubelgiji amesema katika maisha yake alitamani siku moja kucheza sambamba na mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast Didier Drogba, kwa ajili ya kujifunza mengi kutoka kwake, na hii leo hayo yametimia.

Amesema licha ya kutaka kucheza sambamba na Didier Drogba, pia aliipenda sana Chelsea toka kipindi cha mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi Jimmy Floyd Hasselbaink ambae alipata kutamba na klabu hiyo kuanzia mwaka 2000-04.

Amesema akiwa na ndoto hizo aliongeza bidii ya kujituma akiwa uwanjani na kila leo aliwaeleza rafiki zake juu ya kuamini kuitumikia Chelsea katika maisha yake.

Romelu Lukaku alizungumzia ndoto yake alipokua akitambushwa kwa waandishi wa habari, baada ya usajili wake kukamilishwa juma lililopita kwa gharama ya paund million 20.

No comments:

Post a Comment