KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 25, 2011

ARSENAL WATINGA HATUA YA MAKUNDI ULAYA.

Udinese Calcio 1-2 Arsenal FC

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekipongeza kikosi chake kwa kazi nzuri iliyofanyika usiku wa kuamkia hii leo ambayo iliisaidia klabu hiyo kutinga katika hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, baada ya kuwachapa Udinese Calcio mabao mawili kwa moja.

Arsene Wenger ametoa pongezi hizo huku akikiri mambo yalikua magumu katika mchezo huo ambao kila shabiki alikua haipi nafasi kubwa Arsenal kupata ushindi kutokana na hali halisi iliyojitokeza katika michezo iliyopita toka walipoanza msimu kwa kucheza na Newcastle UItd.

Amesema kujituma kwa wachezaji wake pamoja na utulivu katika mchezo wa usiku wa kuamki hii leo, vimekiwezesha kikosi chake kuandika matumaini mapya kwa mashabiki wengi wa soka ulimwenguni kote ambapo sasa wanaingia katika hatua nyingine huku akitazama ni vipi watakavyoweza kukabiliana na mtihani uliopo mbele yao.

Amesema ushindi wa mchezo wa jana pia utafungua mawazo mapya kwa baadhi ya wachezaji wake ambao msimu huu wameanza kuonja joto la mshike mshike wa kukutana na miamba mikubwa barani Ulaya.

Nae nahodha na mshambuliaji wa Arsenel Robon Van Parsie ameongezea jambo katika kauli ya Arsene Wenger kwa kusema ni mwanzo mzuri kwao wa kupata ushindi bila ya kuwa na wachezaji waliopoteza katika kipindi hiki cha usajili.

Arsenal wanatinga katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, kwa jumla ya mabao matatu kwa moja na kuandika historia ya kufaulu kucheza michuano hiyo kwa misimu 14 mfululizo chini ya meneja Arsene Wenger ambae alijiunga na The Gunners mwaka 1996.

No comments:

Post a Comment