KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 30, 2011

ARSENAL KUFANYA USAJILI KABLA YA KESHO !!

Klabu ya Arsenal imeripotiwa kuwa mbioni kukamilisha usajili wa beki wa pembeni kutoka nchini Brazil na klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki Andre Santos na pia wameanza mazungumzo ya kutaka kumsajili beki wa kati kutoka nchini Ujerumani na klabu ya Werder Bremen Per Mertesacker.

The Gunners tayari wameshakamilisha mazungumzo na uongozi wa Fenerbahce na wamekubali kutoa kiasi cha paund million 6.2, kama ada ya uhamisho wa Andre Santos ambae atachukuwa jukumu la kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Gael Clichy alietimkia Man City sanjari na Armand Traore aliekamilisha taratibu za kujiunga na QPR hii leo.

Arsenal pia wamedhamiria kumsajili Per Mertesacker, mwenye umri wa miaka 26, ambapo mishale ya mchana wa hii leo vyombo vya habari vya nchini Uingereza viliripoti kwamba viongozi wa The Gunners pamoja na wale wa Werder Bremen walikua katika mazungumzo.

Kufuatia hatua hiyo kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew, alipasua ukweli kwa kusema amelazimika kumpa ruhusa beki huyo kuondoka kambini, kwa ajili ya kuelekea nje ya nchi kufanyiwa vipimo.


Katika hatua nyingine Arsenal, wamekamilisha hatua za kumsajili nahodha na kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya jamuhuri ya watu wa Korea Park Chu-Young kwa ada ya uhamisho wa paund million 3 akitokea AS Monaco nchini Ufaransa.

Mchezaji huyo anatarajia kutambulishwa kwa waandishi wa habari mara baada ya kurejea katika majukumu ya kitaifa ambapo hii leo timu ya taifa ya jamuhuri ya watu wa Korea inacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Kuwait.

Washika bunduki wa Ashburton Grove, pia wanahusishwa na taarifa za kutaka kuwasajili wachezaji watatu wa klabu ya Chelsea ambao ni Florent Malouda, Alex pamoja na Yossi Benayoun ambapo wote kwa pamoja hawana nafasi ya kujumuishwa katika kikosi cha kwanza cha The Blues.

No comments:

Post a Comment