KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 23, 2011

ARSENAL NA KIWEWE CHA KUWEWESEKA.


Uongozi wa klabu ya Arsenal umewasilisha maombi kwenye shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, ya kutaka adhabu aliyopewa meneja Arsene Wenger icheleweshwe na ikiwezekana awajibike katika majukumu yake hapo kesho katika mchezo wa pili dhidi ya Udinese.

Arsenal wamewasilisha ombi hilo, huku wakiamini UEFA wanaweza kulegeza masharti na kumruhusu mzee huyo wa kifaransa, kujumuika na benchi la ufundi ambalo juma lililopita lilionekana kuhaha hadi kuhitaji msaada wake akiwa jukwaani.

Lakini pamoja na kuomba ombi hilo, bado uongozi wa Arsenal umewasilisha rufaa ya kupinga maamuzi ya kufungiwa michezo miwili kwa meneja huyo, ambae alithibitika kufanya mawasiliano na benchi la ufundi.

Katika mchezo wa kesho Arsenal wanakwenda nchini Italia huku wakiwa na ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata juma lililopita na endapo watahitaji kuendelea, watatakiwa kulinda ushindi huo na pengine kuongeza idadi ya mabao dhidi ya Udinese ambao nao wana kikosi kizuri.

Endapo Arsenal watafanikiwa kupata ushindi, wataingia moja kwa moja katika hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambayo yatapangwa mwishoni mwa juma hili huko nchini ufaransa.

Wakati huo huo klabu ya Arsenal imethibitisha taarifa za kukubali dili la kumuuza kiungo kutoka nchini Ufaransa Samir Nasri, kwenye klabu ya Man City iliyokua ikimuwani kwa kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita.

Arsenal wamekubali dili hilo, zikiwa zimepita saa kadhaa baada ya Samir Nasri kumtaka Arsene Wenger kutomjumuisha katika safari ya nchini Italia, yenye lengo la kwenda kumaliza mchezo wa pili wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Udinese.

Kwa mantiki hiyo sasa Samir Nasri ataelekea mjini Manchester kwa ajili ya kwenda kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilishwa kwa uhamisho wake ambao utaigharimu Man City kiasi cha paund million 22.

Samir Nasri anaondoka Arsenal baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu mitatu ambayo ilishuhudia akicheza michezo 86 na kufunga mabao 18.

Na taarifa zilizopatikana muda mchache uliopita zinaeleza kwamba chama cha soka nchini Uingereza kiziadhibu klabu za Arsenal pamoja na Newcastle Utd kwa kuzitoza faini ya paund 30,000 kufuatai sakata la fujo lililojitokeza katika mchezo wa ufunguzi wa ligi majuma mawili yaliyopita.

Klabu hizo zimeadhibiwa baada ya kuthibitisha kuwa wakuu wa mabecnhi ya ufundi walishindwa kuwatuliza wachezaji.

No comments:

Post a Comment