KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 22, 2011

Arsene Wenger AKUMBWA NA TATIZO JIPYA.

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza kumfungia michezo miwiwli meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger, baada ya kudhihirika alikua akifanya mawasiliano na benchi la ufundi la klabu hiyo wakati wa mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Udinese.

UEFA wametoa adhabu hiyo ambayo itaanza kuchukua mkondo wakati katika mchezo wa siku ya jumatano ambapo Arsenal watasafiri hadi nchini Italia kwa ajili ya mchezo wa pili wa hatua ya mtoano dhidi ya Udinese ambao katika mchezo wa kwanza walikubali kichapo cha bao moja kwa sifuri.

Katika mchezo wa juma lililopita Arsene Wenger alikua anatumikia adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja na UEFA baada ya kumtolea maneno makali muamuzi aliechezesha mchezo wa hatua ya 16 bora msimu uliopita dhidi ya FC Barcelona Macimo Bursacca, alionekana akitoa amri ya kupeleka ujumbe katika benchi la ufundi kupitia kwa kocha wa kikosi cha kwanza cha Arsenal Boro Primorac.

Endapo Arsenal watafanikiwa kupita na kutinga katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, Arsene Wenger ataendelea na adhabu ya kukaa jukwaani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi.

Na endapo Arsenel hawatofanikiwa kupita katika mchezo wa keshokutwa adhabu hiyo itaendelea pia kwa mzee huyo wa kifaransa, ambapo hatoruhusiwa kukaa katika benchi kwenye mchezo wa hatua ya mtoano wa ligi ya barani Ulaya.

Hata hivyo Arsene Wenger amepewa siku tatu za kukata rufaa endapo atataka kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment