KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 22, 2011

Roberto Mancini AWAPIGIA MAGOTI ARSENAL.

Meneja wa Man City Roberto Mancini amelitaka benchi la ufundi la klabu ya Arsenal kutomjumuisha Samir Nasri katika kikosi cha klabu hiyo kitakachocheza mchezo wa pili wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Udinese siku ya jumatano.

Mancini ameomba hivyo huku akiendelea kuamini wakati wowote dili la kumsajili kiungo huyo kutoka nchini Ufaransa litakamilika kwa ada ya uhamisho wa paund million 22 ambalo tayari limeshakubaliwa na Arsenal.

Taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Uingereza vimeeleza kwamba, dili la kiungo huyo limeingia dosari, kufuatia wakala wa Samir Nasri kutaka kulipwa sehemu ya fedha na Man city ikiwa ni makubaliano binafsi.

Mancini amesema endapo Nasri atachezeshwa siku ya jumatano hali itakua mbaya zaidi kwani hatoweza kumtumia kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, ambayo msimu huu itashuhudia kikosi chake kikishoriki kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 1880.

No comments:

Post a Comment