KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 16, 2011

ARSENE WENGER NA WANA ARSENAL.

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger, amemtaka kila shabiki wa klabu hiyo kuamini kwamba hakuna chochote kitakacho wayumbisha zaidi ya kutazama namna ya kusaka mafanikio ya kutwaa mataji msimu huu.

Arsene Wenger ametoa rai hiyo kwa mashabiki wa The Gunners, akiwa katika mkutano wa kuzungumzia mchezo wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya utakaochezwa usiku huu dhidi ya Udanise, ambapo amesema yeye binafsi anaamini hivyo.

Amesema mshikamano na umoja ndio utakaowaongoza, na kufikia malengo waliyojiwekea msimu huu ambao umeanza na matokeo ya sare baada ya kufanya ziara huko mjini Newcastle kwenye uwanja wa St James park.

Msukumo kwa mzee huyo wa kifaransa kuzungumza maneno hayo kwa mashabiki wake ameupata kufuatai maneno mengi kuzungumzwa ikiwa imepita siku moja, baada ya kuondoka Cesc Fabregas alierejea nyumbani, mjini Barcelona nchini Hispania.

Amesema ni kweli wamempoteza mchezaji ambae alistahili kubaki huko Emirates, lakini hakuna budi kutazama mbele na kufungua ukurasa mpya wa maisha.

Arsene Wenger pia ameendelea kulitilia mkazo suala la kutokukubalia kuondoka kwa kiungo kutoka nchini Ufaransa Samir Nasri ambae anahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na Man City.

Amesema kiungo huyo bado yupo na ataendelea kuwepo jijini London na yeye kama meneja wa The Gunners, atapigana kufana na kupona kwa ajili ya kuhakikisha anabaki katika utawala wa Arsenal yenye uchu wa kusaka mafanikio msimu huu.

Arsenal usiku huu wanakwenda katika mchezo wa hatua ya mtoani dhidi ya Udanise kutoka nchini Italia huku wakiamini watafanya vyema kufuatia faida ya kucheza nyumbani kwa mara ya kwanza msimu huu tena mbele ya mashabiki wao.

Katika mchezo huo Arsenal watamkosa nahodha wao mpya Robin Van Parsie pamoja na kiungo Samir Nasri ambao wanatumikia adhabu iliyotolewa na UEFA msimu uliopita.

Arsene Wenger nae ataushuhudia mchezo huo akiwa jukwaani kufuatia adhabu aliyomuangukiwa baada ya kumbwatukiwa muamuzi aliechezesha mchezo wa hatua ya kumi na sita bora dhidi ya FC Barcelona msimu uliopita.

Michezo mingine ya hatua ya mtoano itakayochezwa hii leo ni pamoja na:’

BATE Borisov - Sturm Graz

FC Copenhagen (Denmark) - Viktoria Plzen

Olympic Lyon (Ufaransa) - Rubin Kazan (Urusi)

FC Twente (Uholanzi) - Benfica ( Ureneo)

No comments:

Post a Comment