KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 3, 2011

BABU AMUWEKA SOKO BERBATOV.


Meneja wa Man Utd Sir Alex Ferguson amesema yu tayari kumuuza kiungo mshambuliaji Dimitar Berbatov endapo atapokea ofa ya paund million 20 kutoka kwa vibopa wa nchini Ufaransa Paris St Germain.

Sir Alex Ferguson ameonyesha utayari huyo alipokua akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari mara baada ya mchezo wa jana huko mjini Monaco nchini Ufaransa ambapo kikosi maalum cha Man utd kilicheza dhidi ya Olympique de Marseille na kupokea kisago cha mabao manen kwa mawili.

Amesema yu tayari kutao baraka zote za kuondoka kwa Dimitar Berbatov, lakini endapo kiwango cha fedha alichokitaja kitazingatiwa pasipo kupunguzwa na hii ni kutoka ana umahiri wa mchezaji huyo aliesajiliwa miaka mitatu iliyopita akitokea Tottenham Hotspurs kwa ada ya uhamisho wa paund million 30.75.

Babu huyo wa nchini Scotland akaongeza kwamba, lengo lake kubwa ni kuona Dimitar Berbatov, anacheza kila juma na hataki kumfanyia hiyana ya kukaa benchi, hivyo anachofikiria ni kumpa ruhusa ya kuondoka kutokana na ugumu wa upatikanaji wa nafasi ndani ya kikosi chake.

Dimitar Berbatov, msimu uliopita alifanikiwa kupachika mabao 20 sambamba na mshambuliaji wa Man City Carlos Tevez, lakini alikumbwa na changamoto kubwa ya kujumuishwa kikosini kila mara kufuatia uwepo wa mshambuliaji kinda kutoka nchini Mexico Javier Harnadez Balcazer Chicharito.

Paris St-Germain ambao kwa sasa wapo chini ya muwekezaji kutoka nchini Qatar wamedhamiri kumsajili kiungo huyo kwa lengo la kuendelea kukioboresha kikosi chao ambacho kinaaminiwa huenda kikatwaa ubingwa wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa msimu ujao.

Mpaka sasa klabu hiyo ya jijini Paris nchini Ufaransa imeshafanya usajili wa wachezaji kama Mohamed Sissoko, Salvatore Sirigu, Milan Bisevac, Jeremy Menez , Blaise Matuidi huku kiungo kutoka nchini Argentina na klabu ya Parlemo ya nchini Italia Javier Pastore akiwa mbioni kukamilishiwa uhamisho wake kwa kiasi cha paund million 37.

No comments:

Post a Comment