KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 3, 2011

Breno Rodrigues Borges KUBAKI ALLIANZE ARENA.


Meneja wa mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya soka nchini Ujerumani Bayern Munich Jupp Heynckes ameendelea kusisitiza jambo la kutotaka kukibomoa kikosi chake ambapo mara hii amegusia suala la beki kutoka nchini Brazil Breno Rodrigues Borges ambae anahusishwa na taarifa za kuondoka huko Allainze Arena.

Jupp Heynckes, amerejea tena kutoa msisitizo huo zikiwa zimepita siku chache baada ya kukanusha taarifa za kiungo wake kutoka nchini Ujerumani Bastian Schweinsteiger ambae paia liakumbwa na sakata la kuhusishwa na taarifa za kuondoka siku za hivi karibuni.

Meneja huyo aliekabidhiwa majukumu mara baada ya kuondoka kwa Luis Van Gaaal amesema ni vigumu kwa sasa kufikiaria kumuuza Breno Rodrigues Borges, kutokana na mipango aliyojiwekea kwa ajili ya msimu ujao, na pia ameshangazwa na kuibuliwa kwa taarifa hizo ambazo ameziita ni za kizushi.

Amesema bado beki huyo aliesajiliwa huko Allianze Arena mwaka 2007, akitokea nyumbani kwao katika klabu ya Sao Paulo, ana nafasi ya kujumuishwa kikosini na kusajiliwa kwa beki Jerome Boateng katu hakuwezi kumkosesha nafasi ya kucheza kama ilivyokua siku za nyuma.

No comments:

Post a Comment