KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, August 5, 2011

Daniele De Rossi AREJESHWA KIKOSINI.


Kiungo wa As Roma Daniele De Rossi amerejeshwa katika kikosi cha timu ya taifa baada ya kuachwa msimu uliopita kufuatia sababu za kinidhamu ambazo zilipelekea kufungiwa michezo mitatu ya ligi kuu ya soka nchini humo.

Daniele De Rossi ambae ni miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Italia kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2006 kule nchini Ujerumani, amerejeshwa kikosini huku ikiaminiwa na kocha wa timu ya taifa ya Italia Cesare Prandelli atakua amebadilika kwa kiasi kikubwa.

Nae kipa wa klabu ya Napoli Morgan De Sanctis, ambae hakuwahi kuitwa kikosini toka Prandelli alipokabidhiwa madaraka, amerejeshwa kufuatia kuumia kwa kipa Internazionale Emiliano Viviano.

Kikosi hihco cha Italia pia kimewajumuisha wachezaji wawili kutoka kwenye vilabu vya ligi dajaja lwa pili ambao ni, Angelo Ogbonna wa klabu ya Torino pamoja na Angelo Palombo wa Sampdoria huku wachezaji waliachwa ni washambuliaji Alberto Gilardino, Alessandro Matri pamoja na Marco Borriello.

Kikosi kamili cha Italia ambacho kitapambana na mabingwa wa dunia Hispania katika mji wa Bari siku ya jumatano ya juma lijalo upande wa;

Makipa: Gianluigi Buffon (Juventus), Morgan De Sanctis (Napoli), Salvatore Sirigu (Paris St. Germain)

Mabaki: Federico Balzaretti (Palermo), Leonardo Bonucci (Juventus), Mattia Cassani (Palermo), Giorgio Chiellini (Juventus), Domenico Criscito (Zenit St. Petersburg), Christian Maggio (Napoli), Angelo Ogbonna (Torino), Andrea Ranocchia (Inter Milan)

Viungo: Alberto Aquilani (Liverpool), Daniele De Rossi (AS Roma), Claudio Marchisio (Juventus), Riccardo Montolivo (Fiorentina), Thiago Motta (Inter), Antonio Nocerino (Palermo), Angelo Palombo (Sampdoria), Andrea Pirlo (Juventus)

Washambuliaji: Mario Balotelli (Manchester City), Antonio Cassano (Milan), Sebastian Giovinco (Parma), Giampaolo Pazzini (Inter) pamoja na Giuseppe Rossi (Villarreal).

No comments:

Post a Comment