KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 1, 2011

DIEGO KUCHEZA SOKA HISPANIA.


Aliekua kiungo wa VFL Wolfsburg ya nchini Ujerumani Diego yu njiani kujiunga na klabu ya Atletico Madrid kwa makubaliano ya ada ya uhamisho wa paund million 8.8.

Taarifa zilizotolewa na baba mzazi wa kiungo huyo aliekorofishana na meneja wa VFL Wolfsburg Wolfgang-Felix Magath na kupelekea kufunguliwa milango ya kuondoka huko Volkswagen Arena mwishoni mwa msimu uliopita zimeeleza kwamba kwa sasa mazungumzo ya uhamisho wake yapo kwenye hatua za mwisho.

Djair Ribas da Cunha baba mzazi wa Diego amesema tayari viongozi wa Atletico Madrid wameshafanya mazungumzo na mwanawe na wameafikiana msuala binafsi ya kimaslahi na kinachosubiriwa kwa sasa ni makubaliano ya vilabu husika.

Amesema klabu ya Atletico Madrid itamfaa mwanawe na itampa nafasi ya kucheza kila juma hatua ambayo itapelekea kuendeleza kipaji chake ambacho kilionekana kufifia mara baada ya kundoka Werder Bremen mwaka 2009 na kuelekea nchini Italia kujiunga na kibibi kizee cha Turine Juventus.

Kikosi cha Atletico Madrid ambacho kipo chini ya meneja mpya Gregorio Manzano bado kinaendelea kususkwa, baada ya kuondoka kwa wachezaji kama Thomas Ujfalus aliejiunga na Galatasaray ya nchini Uturuki, Sergio Aguero alijiunga na Man City pamoja na kipa David De Gea aliejiunga na Man Utd.

No comments:

Post a Comment