KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 1, 2011

Wesley Sneijder AKIRI KUWA TAYARI KUJIUNGA NA MAN UTD.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi pamoja na klabu bingwa duniani Inter Milan Wesley Sneijder amekiri kuwa tayari kujiunga na mabingwa wa soka nchini Uingereza Man utd, endapo klabu hiyo itaonyesha nia thabit ya kutaka kumsajili katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa ligi.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, amekiri kuwa tayari kusajiliwa na klabu hiyo akiwa jamuhuri ya Ireland ambapo Inter Milan ilikua ikishiriki michuano ya kuwania ubingwa wa Dublin Super Cup ambapo pia klabu kama Celtic ya nchini Scotland, Man City ya nchini Uingereza pamoja na kikosi maalum cha jamuhuri ya Ireland zilishiriki.

Amesema kwa sasa hawezi kuzungumza lolote juu ya kutaka kusajiliwa na Man Utd, kutokanana taarifa zilizopo kutokua rasmi lakini atafanya hivyo endapo kila kitu kitakua vyema na kufahamika kupitia kwa viongzoi wa klabu yake ya Inter Milan.

Hata hivyo Wesley Sneijder, ametanabai kwamba licha ya taarifa za kutakiwa na Man utd kuendelea kushamiri, bado anajihisi ni mwenye furaha kuendelea kubaki na Inter Milan katika kipindi hiki cha kujiandaa na msimu mpya wa ligi na hadhani kama suala hilo linaweza kumchanganya na akashindwa kufanya shughuli zake nyingine.

Nae meneja wa klabu ya Inter Milan Gian Piero Gasperini, amevitaka vyombo vya habari ulimwenguni kote kuacha kuzusha taarifa za mchezaji wake kuhitajika kwa udi na uvumba huko Old Trafford, ili hali hakuna ukweli wowote juu ya suala hilo.

Amesema mpaka sasa hawajapokea taarifa iliyo rasmi kama Wesley Sneijder, anahitajika kwenye kikosi cha Man Utd na akatoa ushauri kwa waandishi wa habari kusubiri hadi siku ya mwisho ya usajili ambayo ni August 31.

Hata hivyo meneja wa Man Utd Sir Alex Ferguson ameshafunga mjadala wa kiungo huyo kwa kusema hana mpango wowote wa kumsajili.

No comments:

Post a Comment