KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 15, 2011

Giuseppe Rossi AKARIBIA KUREJEA NYUMBANI.

Meneja wa Società Sportiva Calcio Napoli Walter Mazzarri amesema milango ipo wazi kwa ajili ya kumkaribisha mshambuliaji wa kutoka nchini humo pamoja na klabu ya Villarreal ya nchini Hispania Giuseppe Rossi.

Walter Mazzarri amesema mshambulaiji huyo yupo katika mipango yake na ana matumaini makubwa ya kumsajili katika kipindi hiki ikiwa ni sehemu ya kukamilisha mipango yake ya kufanya vyema katika msimu wa mwaka 2011-12 ambao tayari umeshaanza katika baadhi ya nchi barani Ulaya.

Amesema mipango yao kwa sasa ni kutengeza kikosi imara ambacho kitaonyesha upinzani katika michuano ya ndani ya Italia pamoja na ile ya kimataifa hivyo kusajiliwa kwa Giuseppe Rossi itakua sehemu ya kuonyesha namna walivyopania kufanya kweli.

Katika hatua nyingine Mazzarri, amekanusha taarifa za kutaka kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wake huko Stadio Olympico kwa kusema hakuna mchezaji hata mmoja ambae atauzwa klabuni hapo katika kipindi hiki cha usajili ambacho kitafikia kikomo August 31.

Wachezaji wanahusishwa kuondoka huko Stadio Olympico ni Edison Cavani, Marek Hamsik pamoja na Ezequiel Lavezzi ambae anasemekana kuondoka kwake kutasababishwa na ujio wa Giuseppe Rossi.

No comments:

Post a Comment